Pages

Saturday, March 1, 2014

DALILI ZA MUME ANAETEMBEA KIMAPENZI NA HOUSE GIRL (dada wa kazi)

DALILI YA KWANZA
Ishara ya kwanza ya mwanaume ambaye tayari
yupo ndani ya uhusiano wa kimapenzi na
msichana wa kazi ni kupenda sababu za
kumwamsha mfanyakazi huyo  hata pale
anaporudi na kumkuta amelala.
Utakuta baba amerudi nyumbani usiku wa saa
sita, mkewe anamfungulia mlango, akishaingia na
kukaa, anaanza:
“Dada amelala?”
Mke: “Ndiyo.”
Baba: “Mwamshe nimpe kazi f’lani.”
Mke unaweza ukamtetea sana msichana, lakini
mumeo akasimamia msimamo ule ule.
Sasa utakapomwamsha, akifika, mumeo
utamuona anavyojipinduapindua.
“Hii mboga umepika wewe dada?”
“Hapana, mama.”
“Ooo. Ulifua zile soksi zangu?”
“Ndiyo baba.”
“Sawa kalale.”
Mke unajiuliza, sasa kumwamsha kote kule ndiyo
maswali yenyewe hayo tu.
Sasa tuendelee…
Katika hali kama hii, wewe mke jaribu kuwa
makini sana. Hakikisha hutoi nafasi kwa mumeo
kumfikia au kuwasiliana na hausigeli kwa kitu
chochote. Kama ni maji ya kuoga tenga wewe,
vitu ambavyo vinawezekana kufanywa na wewe
vitimize ili kuukata uhusiano hata kama utakuwa
hujathibitisha kama upo!
Tatizo kubwa ni kwamba, wanawake wengi siku
hizi wanawafanya wasichana wa kazi ndiyo
wenye nyumba, wao wasaidizi, wakati zamani,
hausigeli ndiye msaidizi wa kazi za ndani, mambo
mengine yote ni kwa akina mama wenyewe.
DALILI YA PILI
Ishara hii inatakiwa mke mwenye utambuzi sana,
yaani awe na ufahamu wa hali ya juu vinginevyo
anaweza kukurupuka na kumbwatukia mumewe
kumbe hana habari na msichana wa kazi.
Ila kwa wale ambao wana uhusiano sasa,
ukimwona mumeo ana tabia ya kuchelewa kulala
eti yupo sebuleni, mke changamka, hapo pana
jambo.
Mume anayefanya hivyo hutoa nafasi kwa mkewe
kwenda kulala na yeye kunyatia chumbani kwa
hausigeli kuduu naye.
Sasa endapo mke utakwenda sebuleni na
kumkuta mumeo anajifanya kukodolea macho
tivii ili ujue anaangalia vipindi, jaribu na wewe
kuchunguza aina ya kipindi, ukikuta ni taarifa ya
habari ya Sky News,CCTV, CNN, BBC au Al
Jazeera, ujue huyo mwongo tu, hana lolote.
Lakini usiishie hapo, jifanye na wewe unakaa
pembeni yake kuangalia taarifa hiyo ya habari.
Utamuona yeye anasimama na kusema…
“Tukalale mke wangu.”
Kama wakati wa kwenda kulala wewe
utatangulia, yeye lazima aingie chooni kwanza,
anajifanya anajisaidia haja ndogo lakini
anachotaka ni wewe uingie chumbani, yeye
aingie kwa hausigeli ili ampige busu japo moja
tu, maana anajua dili limeshatibuka.
Lakini dalili hii ni kwa mume ambaye hapo
nyuma hakuwa na tabia ya kukaa sebuleni peke
yake na kuangalia tivii.
Kwa upande wa hausigeli aliye katika uhusiano
na baba mwenye nyumba, huwa hivi…
Wakati baba amekaa sebuleni usiku akiangalia
tivii ‘kiuongo’, yeye anaosha vyombo nje, tena si
ajabu amevitawanya kiasi kwamba, kama ni
kumaliza ataweza kwenda hasi usiku wa manane.
Na kila baada ya dakika tano, msichana huyo
ataingia ndani na kupita mbele ya baba. Lengo
lake ni kusoma mazingira kama mama mwenye
nyumba amelala.
Kwa vile wao si waanzaji (kama ilivyo tabia ya
mwanamke), basi unaweza kumwona
anashikashika vitu vya sebuleni, kama vile
kuweka sawa vitambaa vya makochi (japo ni
usiku), kufuta meza, kabati au wakati mwingine
kupanga CD za muziki au filamu ambazo zipo
kwenye shelfu lake. Mambo hayo anayafanya
huku vyombo vikimsubiri nje!
Hapo anachotaka, baba amuone kirahisi na
kuanza kumtekenya-tekenya, kumshika-shika
hatimaye ‘kumalizana’.
Utashangaa, ukifuatilia sana, utakuta hausigeli
akishamalizana na mume, vyombo anaviingiza
ndani na kuvimalizia kesho yake asubuhi.
Kwa maana hiyo pia, wake za watu wawe macho
na wasichana wa kazi wanaoshindwa kumaliza
kuosha vyombo usiku.
MAENEO YA UFUSKA
ni vyema niweke wazi maeneo ambayo ma-baba
wenye nyumba ndiyo hupenda kutumia kufanya
mapenzi na wasichana wa kazi.
Ni vigumu sana kukuta wawili hao wanamalizana
sebuleni (ingawa inawezekana sana) kwani ni
eneo hatari kuliko yote ndani ya nyumba.
Uchunguzi wa kina wa kimazingira umegundua
kuwa, kati ya maeneo hatari kwa fumanizi ndani
ya nyumba ni sebuleni.
Wengi waliowahi kufumaniwa, mfano mume kula
uroda na shemeji yake (mdogo wa mkewe) au
binti kuliwa uroda na hausiboi, ilikuwa sebuleni.
Aidha, sebuleni ndiyo mahali panapofikwa kwa
mara ya kwanza na watu waliolala ndani ya
nyumba kuliko sehemu nyingine yoyote.
Kwa hiyo, mababa wengi sasa hukwepa sebule
na kwenda chumbani kwa msichana, stoo,
bafuni, jikoni kama liko pembeni na uani, hasa
maeneo yenye vificho kama nyuma ya karo au
kama kuna sehemu kumesimamishwa vitu
chakavu.
Chooni si sana kwa sababu ni eneo linalofikwa na
watu kila wakati karibu usiku kucha.
Sasa hatari ipo hivi, mke asiyejua haya, kama
mumewe ataendelea kimapenzi na hausigeli,
hufikia wakati uhama nyumba. Namaanisha
kwamba, hufika mahali wakitaka kukutana
kimwili, wanakwenda gesti.
Gesti zao mara nyingi ni nyuma ya nyumba au
mtaa wa pili, huwa hawaendi mbali sana kwa
kuogopa muda wa msichana kufanya kazi za
ndani.
Tutaendelea wiki ijayo. jamani, tuone dalili ya
tatu.

KIDOGORO USWAZII

Jiji la
dar es salaam huwa ni tamu lakini lina kero zake na
uenda kero ni nyingi kuliko raha zilizopo… moja wapo ya
kero kubwa zaidi ni hili ambalo bila shaka kila mmoja
wetu anayeishi uswahilini linamgusa kwa namna moja
ama nyingine … si linguine ni swala hili la miziki ya
kukesha ambayo imejichukulia umaarufu kwa jina la
vigodoro, kwa mtu anaye kaa mitaaa ya mbezi beach,
upanga au masaki ni vigumu kuelewa nachomaanisha
lakini kwa watu wa yombo vituka, tandale kwa tumbo ,
ukonga mazizini na sehemu kama tandika wananielewa
vizuri…
Ni ukweli usiopingika kuwa hii ni kelo ya watanzania
wengi hapa jijini, mara nyingi miziki hii uanza siku ya
alhamisi au ijumaa na kwenda mpaka jumapili… kero hii
inatokana na mtindo wa upigaji wa mziki huu usiozingatia
mda ambapo upigwa mpaka asubuhi bila kujali usumbufu
mkubwa wanoupata watu wa karibu na vigodoro hivyo…
sasa pata picha umerudi toka kazini sa tano usiku
kutokana na foleni iliyopo mjini na unaamua kujipumzisha
kidogo ili uwahi kuamka ukatafute riziki… kwa sauti ya
mziki huu sidhani kama utapata usingizi … kitu ambacho
kinaweza kupelekea uamke umechoka na ushindwe
kufanya kazi zako kwa ufasaha,,,, hapa tunaweza kusema
kwamba miziki hii inarudisha nyuma maendeleo ya
watanzania nan chi kwa ujumla. Kero nyingine ya miziki
hii ya usiku ni ukiukwaji wa maadili ya mtanzania kwani
kubali ukatae watu wanacheza bila kuhofia chochote na
mara nyingi kama unavyojua nyumba zetu za uswahilini
wengi hatuna mageti ya kuwazuia watoto wetu… watoto
wengi wa umri wa chini ya miaka kumi na nane
wamekuwa wakitoroka nyumbani na kukimbilia kwenye
vigodoro hivo na kuwafanya wajifunze tabia ambazo ni
zaidi ya umri wao.
Nadhani imefika wakati sasa serikali kuangalia upya
sharia za upigaji mziki katika kumbi za starehe na
majumbani.. mara nyingi sharia inasema baa zifungwe sa
sita labda uwe na kibali naalum kutoka sehemu husika ..
lakini hii imekua ni tofauti kwa vigodoro kwani uenda
mpaka asubuhi na kusababisha kero isiyokuwa ya
kawaida kwa wakazi wa maeneo ya uswahilini

Friday, February 21, 2014

Uarabuni utanyongwa

BREAKING NEWS, MATOKEO KIDATO CHA NNE YATANGAZWA, 58% WAFAULU

Shule 10 bora matokeo kidato cha nne
2013
ni:
1. St.Francis Girls (Mbeya)
2. Marian Boys (Pwani)
3. Feza Girls (Dar-es-salaam)
4. Precious Blood (Arusha)
5. Canossa (Dar-es-salaam)
6. Marian Girls (Pwani)
7. Anwarite Girls (Kilimanjaro)
8. Abbey (Mtwara)
9. Rosmini (Tanga)
10. DonBosco Seminary (Iringa)

Thursday, February 20, 2014

JE UNAMKUMBUKA HUYU KIJANA ALIE TIKISA KWA HIZI PICHA ZAKE ZA UCHAFU....ANAITWA MANAIKI SANGA NA CHAKUSHANGAZA ALIKAMATWA NA UNAAMBIWA YUPO URAIANI ANAENDELEZA USHEITANI WAKE KAMA KAWAIDA

ALIYEZAA NA SHILOLE AIBUKA

KWA mara ya kwanza, mzazi mwenza
na msanii wa muziki na filamu Bongo ,
Zuwena Mohamed ‘ Shilole ’ , Elias
Makala ameibuka na kujinadi hadharani
wilayani Igunga, Tabora.

Tukio hilo lilitokea Februari 14 , mwaka
huu ( Valentine’ s Day ) ambapo Shilole
aliyekuwa amekwenda kufanya shoo
mkoani humo , alishindwa kuzuia hisia
zake baada ya mzazi mwenzake huyo
kujitokeza na kujikuta wakioneshana
mahaba mbele za watu .
Pozi hilo la kimahaba liliwashangaza
watu na kuanza kudhani kuwa huenda
wawili hao wakarudisha penzi lao
lililokufa miaka mingi iliyopita .
“Mh! Kweli mtalaka hatongozwi , hebu
ona Shilole alivyorembua alipomuona
jamaa yake, pale Makala kumchukua ni
kama kumsukuma mlevi , ” alisema
shuhuda mmoja .

Baada ya paparazi wetu ‘ kuusoma
mchezo ’ huo , aliamua kumuuliza staa
huyo kama penzi lao limerudi upya au
laa ?
“Hahahahaa! Kwa kweli unanichekesha
kuniuliza kama nimerudisha penzi kwa
mzazi mwenzangu, huyu ni baba wa
mwanangu Joyce , itabaki kuwa hivyo .
Siwezi kumtenga na sioni ajabu kupiga
naye picha, hakuna kinachoendelea , ’’
alisema Shilole .
Licha ya kufafanua hivyo , usiku wa siku
hiyo, Shilole alipokuwa jukwaani
akipagawisha mashabiki kwa shoo kali ,
alimpandisha jukwaani mzazi mwenziye
huyo hali iliyozua mtafaruku mkubwa
kwa mpenzi wa sasa wa Makala
aliyefahamika kwa jina la Maguno .
Baada ya shoo kuisha , Maguno
aliyekuwa na jazba kwa mpenzi wake
kupandishwa jukwaani , alimsaka Shilole
kwa udi na uvumba kutaka
kumtembezea kichapo lakini bahati
haikuwa yake, hakuweza kumpata hadi
msanii huyo aliporejea jijini Dar siku
iliyofuata.

Wednesday, February 19, 2014

Thubutu kuvalia 'Mini Skirt' Uganda!...miaka 10 jela

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia
saini sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa
wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu
uchi au kuhusika na vitendo vinavyohusisha
picha zenye watu uchi.
Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia
sketi fupi sana au 'Mini Skirt' kama
zinavyojulikana au blausi ambazo
zinaonyesha kifua chao hadharani na
kusababisha hisia za kingono .
Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo
zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya
mafunzo au wakati wa michezo na hafla za
kitamaduni.
Akihutubia waandishi wa habari, mjini
Kapmala, waziri wa maadili na utawala
bora, Reverend Simon Lokodo alisema kuwa
Rais Museveni alipitisha sheria hiyo tarehe
6 mwezi huu, miezi mwili bada ya bunge
kuipitisha.
Kwa mujibu wa sheria hiyo kamati dhidi ya
vitendo hivyo itabuniwa ili iweze kutekeleza
sheria hiyo kwa kuhakikisha kuwa picha, au
video zenye watu uchi zinanaswa na
kuharibiwa.
Kamati hiyo, itajumuisha watu kutoka
katika sekta mbali mbali ikiwemo ya habari
na utumbuizaji.
Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote
atakayepatikana akijihusisha na vitendo cya
watu kuwa uchi, kuvalia nusu uchi , kuona
sinema za watu wakiwa uchi au kuchapisha
picha za watu walio uchi kwa lengo la
kuleta hisia tofauti utachukuliwa hatua kali
za kisheria.
Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu
kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua
hisia zisizofaa miongoni mwa watu.
Watakaopatikana wakivunja sheria na
kuvalia visivyo watafungwa hadi miak 10 na
wale watakaopatiokana na hatia ya
kuhusisha watoto katika biashara ya ngono
watafungwa hadi miaka 15.

Total Pageviews

NeoCounter