Pages

Wednesday, June 13, 2012

Mama Wema atakiwa kufunga mdomo

Mama mzazi wa miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ametakiwa kufunga mdomo kwa kumwongelea mwanaye hasa kwenye matatizo yake na mastaa wenzake.
Hayo yamezemwa na watu kwa kutumia mtandao wa bbm ambapo watumaji walikuwa wakimshauri mwanamke huyo baada ya matamshi yake ya siku ya jumanne ambapo alimchana msanii mpinzani na mwanaye, Jackline wolper.
Katika maelezo yake ambayo yalitolewa kwa sehemu kwenye kipindi cha take one cha zamaradi mketema, mama wema alimgusia wolper kwa kusema kwamba asimseme mwanaye kuhusu pa kulala kwani anapo na pazuri sana.
Watu walioangalia kipidni hicho walimtaka mama huyo kuachana na mambo ya watoto kwani mastaa wa bongo ndiyo zao, leo wanakuwa marafiki, kesho hapakaliki.Kwa upande wake Wolper alisema hajui nini kinaendelea kati yake na wema kwani yeye anaishi maisha yake na hamfuatifuati mtu, lakini  kila kukicha anasakamwa.
“Mimi sijui nini kinaendelea, mbona naishi maisha yangu mwenyewe, lakini kila kukicha nasemwa vibaya, da!” alisema Wolper.
Nilimsikia Mama Wema alivyonipasha maana ilikuwa bonge la mpasho. Mimi siwezi kujibizana na mama yakeWema, yeye ni kama mama yangu maana ana umri mkubwa kumzidi hata mama yangu mzazi, kujibizana nae ni kujivunjia heshima na kumvunjia heshima yeye pia, hilo sintaweza kabisa dada Irene!

Japo naona ingependeza mama yetu huyu angetuita na kutuweka chini kujua nini tatizo. Mimi nina wazazi na nina ndugu lkn hata siku moja hawawezi kabisa kwenda kwenye vyombo vya habari na kuongelea au kuingilia ugonvi wa mimi namarafiki zangu.


Kuna siku nyingine Irene Uwoya na huyo Wema walikwenda kunitukana kwenye Tv fulani. hiyo pia nilidharau, sipendi kujidhalilisha kwa maneno maneno ya mitaani nisiyojua hasa yanalengo gani! nina shughuli nyingi za kufanya kamwe siwezi kujibizana nao.

alisema Jaque.
 
 
kwa hisani ya; irenemwamfupejamii.blogspot.com


2 comments:

Total Pageviews

NeoCounter